Sunday, January 6, 2008

Yanga-Tumerudi na silaha za maangamizi

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Imani Maugila Omar Madega akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari nchini hivi karibuni.

Na Adolph Balingilaki, Julius Kihampa

Baada ya kurejea nchini kutoka katika ziara ya kimafunzo kikosi cha wachezaJI 27 wa Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam kimeahidi kufanya maangamizi makubwa katika mzungumko wa pili wa Ligi kuu Tanzania Bara na michuano ya kombe la Shirikisho ya Afrika.

Akizungumza na Championi juzi katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam,Nahodha wa timu hiyo,Fred Mbuna alisema kuwa kile walichoenda kukifanya kimekamilika wanachosubiri ni kuingia vitani na kuanza kushambulia maadui wanaowazungumka.

"Kazi tukiyotumwa tumeikamilisha tunasuburi kuanza kushambulia kila adui atakayekuja mbele yetu,huu sio wakati wa kuzungumza maneno matupu tunaingia vitani tukiwa na lengo moja kushinda vita"alisema Mbuna.

Nahodha huyo aliyeongoza kikosi cha vijana wa Jangwani kikiwa chini ya Kocha Mkuu Dusan Kodic akiwa na msaidizi wake Spaso Sokolovski aliongeza kuwa wakiwa nchini Afrika Kusini wamepata mbinu mpya za kupigana sehemu yoyote ya uso wa dunia.

Mbuna alisisitiza kuwa wachezaji wamekuwa makini na mafunzo waliyokuwa wakipewa na walimu huku wakiwa na kumbukumbu ya kutaka kumaliza uteja wa kufungwa na watani wao wa jadi Simba.

"Dawa ya Simba tumekuja nayo kutoka Bondeni,siwezi kusema jina lake lakini nakuomba usubiri mambo makubwa mwaka huu,atuwezi kuwa wataja wa watu wanaolia njaa kila siku, hiyo iatkuwa dharau na mungu apendi"alisisistiza Mbuna.

Naye Katibu Mwenezi wa Yanga,Francis Lucas akizungumza na Championi alisema kuwa nia na malengo ya safari yametimia wanachosubiri ni vijana kuanza kufuna walichopanda katika ardhi yeye rutuba.

"Tumetumia gharama kubwa kuweka kambi kuanzia Mwanza hadi huko nchini Afrika Kusini,tunataka kuona kile ambacho tumekipanda kama kitaota kama tunavyotaka,wakati wa ubabaishaji umekwisha tunataka mafanikio zaidi"alisema Francis.

Katibu Mwenezi huyo aliongeza kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Dusan Kodic hakupenda kucheza mechi ngumu kutoka na kutaka wachezaji wake waweze kupata maelekezo yake kwa ufasahaz zaidi.

Timu ya Yanga imerejea nchini ikiwa na kibarua kigumu cha michuano ya kombe la Mapinduzi inayoanza kesho katika dimba la Amani huko Tanzania Visiwani(Zanzibar) huku ikisubiri kuanza mchakamchaka ya duru la pili la Ligi Kuu Tanzania Bara Januari 26 mwaka huu.

No comments: