Na Violet Mushi
Kiungo mchezashaji wa Timu ya Moro United, Ally Yusuph 'Tigana' amesema kuwa amekamilisha mipango ya kwenda kufanya majaribio ya kusakata soka la kulipwa huko nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na Championi mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam,Tigana alisema kuwa Wakala wake amekalimisha kila kitu kinachotakiwa kwa ajili ya majaribio hayo kwenye klabu ya Jomo Cosmos.
"Ninasumbiri kupata ruhusa kutoka kwa viongozi wangu wa Moro, siku na wakati wowote nitaondoka zangu kwenda huko Bondeni kusaka maisha mapya"alisema Tigana.
Mchezaji huyo aliyewahi kuchezea timu za Yanga na Simba kwa nyakati tofauti, aliongeza kuwa ana imani ya kufanya vizuri katika majaribio hayo yatakayochukua wiki tatu.
Tigana alisisitiza kuwa yupo tayari kurejea kwenye klabu yake ya Moro United kwa ajili ya mzungumko wa pili wa Ligi kuu Tanzania Bara iwapo mambo yatakuwa ndivyo sivyo.
Sunday, January 20, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment