Sunday, January 20, 2008

Twiga Stars uso kwa uso na Zimbabwe

Na Eunice Macha

Timu ya Taifa ya Soka ya wanawake Tanzania Bara Twiga Stars wanatarajia kupimana na timu moja kutoka Zimbabwe kabla ya mpambano kati ya watani wao wa Cameroon.

Akizungumza na Championi juzi Katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela alisema timu hiyo itachuana na timu moja kutoka Zimbabwe kwa sababu nchi hiyo inawataalamu waliobobea soka.

Alisema kuwa, Twiga Stars ni timu nzuri ya wanawake lakini bado wanahitaji tiu kubwa kwa ajili ya kujipima zaidi ili soka hilo liweze kuendea kwa kasi hapa nchi.

"TFF tunataka timu yetu ya wanawake iwe sawa na timu ya Taifa Stars, hatutaki kusikia Tanzania hakuna soka la wanawake, sisi tunachotaka ni kusikia Tanzania inaongoza kwa soka la wanawake na wanaume,"alisema Mwakalebela.

Mwakalebela alisema kuwa, wameamua kutafuta mechi ya kirafiki kutoka Zimbabwe kabla ya mpambano kati yao na Cameroon kwa sababu timu hiuyo ya Cameroon wana stamina kubwa kuliko Twiga Stars.

"Timu ya Cameroon ipo juu sana kisoka ingawa hata Twiga Stars wapo juu lakini kuna kuzidiana, hivyo kutokana na uwezo wa Cameroon itabidi timu yetu ijipime kwanza na timu moja kutoka Afrika kusini pamoja na Zimbabwe na baada ya hapo ndio wapambane na watani wao," alisema Mwakalebela.

Alisema kuwa, TFF bado inaendelea kukusanya vipaji vya soka la wanawake kwa sababu, Tanzania ni nchi ambayo ipo nyuma kwa upande wa soka la wanawake tofauti na nchi nyingine.

No comments: