Sunday, January 27, 2008

Serikali yawashukia Makocha wazawa





Picha ya kwanza hadi ya nne ikionesha pozi tofauti za Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Seif Muhamed Khatib, picha mbili za mwisho akiwa na mwandishi wa safu ya face 2 face ya gazeti la Championi, Ahadi Kakore wakati wa mazungumzo baina yake na mwandishi huyo hivi karibuni ofisini kwake.(Picha na Christopher Lisa wa Global Publishers)


Na Ahadi Kakore

Serikali imesema kwamba klabu za Tanzania kufundishwa na makocha wa kigeni zaidi ya wazawa si suala geni bali jambo lillilozoeleka kwa miaka mingi katika soka la Tanzania.

Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Seif Muhamed Khatib, ameiambia Championi kati kati ya wiki hii kwamba makocha wazalendo wanatakiwa kuacha kulalamikia hatua hiyo kwani suala hili lilikuwepo hata kabla ya kipindi hiki.

Khatib ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa timu ya Caltex FC na timu ya Taifa ya Zanzibar, alisema kuwa makocha wazawa wanatakiwa kujiendeleza kielimu zaidi ili kulingana au kuwazidi hao wanaotoka nje.

Aliongeza kuwa suala la kucheza mpira si kigezo pekee cha kumfanya mtu kuwa kocha ila elimu na uwezo wa kufundisha ndivyo vitu vinayoweza kumfanya kocha kuwa bora.

"Suala la Timu za Taifa na klabu kufundishwa na Makocha kutoka nje si jambo la leo wala jana ila kinachotakiwa kwa makocha Wazalendo ni kujiendeleza zaidi kwa sababu wanaweza wakalalamika lakini wakawa hawana sifa kutokana na elimu zao kwa maana kila mtu duniani anahitaji kilicho bora," alisema Khatib.

Katika hatua nyingine Khatib alisema kwamba ari ya ushindani ya kutafuta makocha bora inayofanywa na klabu za Tanzania ni moja ya hatua ya maendeleo, ila wadau wa soka wanatakiwa kuwa wavumilivu kwani wengi wanataka mafanikio ya haraka kitu ambacho hakiwezekani kufanyika mara moja.

Klabu pekee nchini ambayo imejaza makocha wa kigeni ni Yanga ya jijini Dar es Salaam, ambapo hadi hivi sasa inamakocha wanne wa kutoka nje ya Tanzania ambao ni, Dusan Kondic, Spaso Sokolovsk, Zivojnov Srdan wote kutoka Serbia na Mmalawi Jack Chamangwana.

Thursday, January 24, 2008

Haya ndiyo maisha ya David Beckham nchini Marekani

1.Hili ndilo jumba la kifahari analioishi
2.Mkewe Beckham anaitwa Victoria maarufu kama Posh.
3.Picha mbali mbali za mkali huyo wa LA Galaxy.

(1)

(2)(3)

Sunday, January 20, 2008

Dalali ampa somo Boban

Na Eunice Macha

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Hasan Dalali ametoa somo kwa mshambualiaji mahiri wa Timu ya hiyo na Taifa Stars, Haruna Moshi Boban kuwa mvumilivu wakati wa mechi za ligi kuu soka Tanzania Bara mzunguko wa pili ili kuepuka kufungiwa tena.


Akizungumza na Championi mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Dalali alisema kwamba anamshauri Boban kuwa mvumilivu na maamuzi yanayotokea uwanjani ili kuepuka kukumbana na adhabu za TFF.

Aliongeza kuwa uwezo wa Boban ni mkubwa na kila mtu analijua hilo lakini kukosekana kwa uvumilivu kunaweza kusababisha kuidhoofisha timu kwani mchango wake ni muhimu kwa Simba na kwa taifa.

Aidha alifafanua kuwa maamuzi katika baadhi ya viwanja hapa nchini hayapendezi na yanakatisha tamaa kwa wachezaji lakini wanatakiwa kuwa wavumilivu kwa kutowapiga wala kuwatukana waamuzi kwani itasaidia kuondoa adhabu mbali mbali ikiwemo kufungiwa.

"Mimi Bobban nampenda sana kwa sababu anacheza kwa kujiamini, na stamina yake inamruhusu kucheza hata soka la Kimataifa ila tatizo lake ni hilo la kutokuelewana na baadhi ya waamuzi tu", alisema Dalali.

Haruna Moshi 'Boban' alifungiwa na kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka nchini TFF muda wa miezi mitatu kwa kosa la utovu wa nidhamu hivyo kukosa baadhi ya mechi za mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara vile vile alikosa kucheza michuano ya CHALENJI ambapo Stars haikufika popote.

Ebwanee! Tigana atimkia kwa Mbeki

Na Violet Mushi

Kiungo mchezashaji wa Timu ya Moro United, Ally Yusuph 'Tigana' amesema kuwa amekamilisha mipango ya kwenda kufanya majaribio ya kusakata soka la kulipwa huko nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na Championi mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam,Tigana alisema kuwa Wakala wake amekalimisha kila kitu kinachotakiwa kwa ajili ya majaribio hayo kwenye klabu ya Jomo Cosmos.

"Ninasumbiri kupata ruhusa kutoka kwa viongozi wangu wa Moro, siku na wakati wowote nitaondoka zangu kwenda huko Bondeni kusaka maisha mapya"alisema Tigana.

Mchezaji huyo aliyewahi kuchezea timu za Yanga na Simba kwa nyakati tofauti, aliongeza kuwa ana imani ya kufanya vizuri katika majaribio hayo yatakayochukua wiki tatu.

Tigana alisisitiza kuwa yupo tayari kurejea kwenye klabu yake ya Moro United kwa ajili ya mzungumko wa pili wa Ligi kuu Tanzania Bara iwapo mambo yatakuwa ndivyo sivyo.

Twiga Stars uso kwa uso na Zimbabwe

Na Eunice Macha

Timu ya Taifa ya Soka ya wanawake Tanzania Bara Twiga Stars wanatarajia kupimana na timu moja kutoka Zimbabwe kabla ya mpambano kati ya watani wao wa Cameroon.

Akizungumza na Championi juzi Katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela alisema timu hiyo itachuana na timu moja kutoka Zimbabwe kwa sababu nchi hiyo inawataalamu waliobobea soka.

Alisema kuwa, Twiga Stars ni timu nzuri ya wanawake lakini bado wanahitaji tiu kubwa kwa ajili ya kujipima zaidi ili soka hilo liweze kuendea kwa kasi hapa nchi.

"TFF tunataka timu yetu ya wanawake iwe sawa na timu ya Taifa Stars, hatutaki kusikia Tanzania hakuna soka la wanawake, sisi tunachotaka ni kusikia Tanzania inaongoza kwa soka la wanawake na wanaume,"alisema Mwakalebela.

Mwakalebela alisema kuwa, wameamua kutafuta mechi ya kirafiki kutoka Zimbabwe kabla ya mpambano kati yao na Cameroon kwa sababu timu hiuyo ya Cameroon wana stamina kubwa kuliko Twiga Stars.

"Timu ya Cameroon ipo juu sana kisoka ingawa hata Twiga Stars wapo juu lakini kuna kuzidiana, hivyo kutokana na uwezo wa Cameroon itabidi timu yetu ijipime kwanza na timu moja kutoka Afrika kusini pamoja na Zimbabwe na baada ya hapo ndio wapambane na watani wao," alisema Mwakalebela.

Alisema kuwa, TFF bado inaendelea kukusanya vipaji vya soka la wanawake kwa sababu, Tanzania ni nchi ambayo ipo nyuma kwa upande wa soka la wanawake tofauti na nchi nyingine.

TFF kukutana Machi

Na Shufaa Lyimo

Shirikisho la soka Tanzania TFF linatarajiwa kufanya mkutano mkuu wa kujadili mambo mbali mbali ya soka mwanzoni mwa mwezi March mwaka huu.

Akizungumza na Championi hivi karibuni Rais wa Tff Leodgard Tenga alisema kuwa,lengo na dhumuni la kufanya mkutano huo ni kutaka kupanua soka zaidi hasa kwa vijana wadogo wanaochipukia sasa hivi.

Hata hivyo tutajadili mambo mbalimbali ya kuboresha soka Tanzania ikiwa ni pamoja na kutafuta njia za kufanya ili vilabu vyetu viwe na sifa mojawapo ya kuepukaka migogoro inayojitokeza mara kwa mara katika klabu zetu.

"Katika mkutano huo tutahakikisha tutakaalo lizungumza tutalifanyia kazi na kuboresha soka nchini Tanzania kama jinsi wenzetu wanavyofanya katika nchi zao kwa kuweka soka kuwa kipao mbele" Alisema Tenga.

Vile vile aliendelea kusema kwamba, sasa hivi Tanzania imepanuka sana kisoka na katika kikao hicho watafanya mambo ambayo yatawabadilisha viongozi mbali mbali wa Klabu na kuwaletea mafanikio makubwa.

Sunday, January 13, 2008

Pata ujumbe wa Mapenzi kisha mtumie yule unayempenda

Picha kwa hisani ya http://www.datingsiteportal.net


Sikia wimbo huu, Mapenzi

Mapenzi ni zaidi ya fikra,
Mapenzi ni kama mchezo,
Mapenzi ni zaidi ya chochote juu yako,

Kwa kila kitu na siku zote,
Mapenzi kama zaidi ya tabasamu tamu,
Mapenzi ni kama wimbo mtamu,

Mapenzi ni zaidi ya hisia,
Ni zaidi ya mawazo,
Mpenzi nibebe tuwe pamoja kama kumbikumbi,

Nakupenda kwa MOYO ,
Mwiliwangu na damu yangu nitakupa,
Napenda unavyonionesha njia za mapenzi,

Hakika sijiwezi kwa mapenzi yako,
Nakumbuka wakati tukiwa pamoja,
Nakumbuka jinsi unavyonitazama,

Nakumbuka unavyoniambia, nikushike,
nikulambe nami nilifanya, kiba hiyana,
Hakika nakupenda kwa kila hali,

Endelea kuniita MPENZI nani nikuite ASALI,
Nakutamkia tena na tena, NAKUPENDA,
Na siwezi kukusaliti milele.


Haiba ya Moyo

Ni kweli wewe ni mwanamke wa pekee,
Umebarikiwa mambo mengi matamu pekee,

Ndimi zako laini, tamu zisizo na mfano,
Mguso wako ni waajabu na wenye ubaridi,
Nikiwa nawe napoteza kumbu kumbu,

Nakiri kusema nikiwa nawe ni zaidi ya mbumbumbu,
Mapigo ya moyo wako yanadunda kifuani mwangu,

Sawa na upepo baharini usiokoma kuvuma,
Nakuwaza kila iitwapo asubuhi,

Na hunijia ndotoni nyakati za usiku,
Nguvu ya mapenzi yako ni zaidi ya silaha za sumu,

Na kamwe siwezi kusimulia utamu wa hazina ya asali yako,
ILA NITAKUPENDA daima.



Hiki ni moja ya vitabu vinavyozungumzia masuala ya mapenzi wa undani kitafute upate mengi


Mwanamke wa maisha nyangu

Wewe ni mwanamke wa maisha yangu,
Wewe ni Malkia ndani ya moyo wangu,

Mimi ni madini kwenye ngao kichwani mwako,
Wewe ni Jua liwakalo na kunipa mwanga mchana,

Pia hunipa joto nyakati za usiku,
Kadhalika u-miale ya jua la subuhi,

Unataka nikwambie nini kipya?,
Naam pokea ujumbe huu kutoka kwangu wakati huu,

Mimi ni mawingu sahihi ndani ya kifua chako kitamu,
Mimi ni mto upishao maji halisi na masafi yaitwayo MAPENZI, Umenielewa?

Wewe ni mlima wenye kilele kirefu ulijaa kila ainaya raslimali,
Japo mmiliki ni mimi lakini wengu wanalitamani,

Naahidi kukulinda na kila aina ya uvamizi dhidi yako,
Sitaki mtu afyeke na kuchoma moto msitu wako wa uletao mmvua iitwayo mapenzi,


Jina lako

Nimeandika jina lako angani,
Lakini mawingu yanelibeba,

Nimeandika jina lako hewani,
Lakini upepo umelichukua,

Nimeandika jina lako katika MOYO wangu,
ambalo lipo na litaendelea kuwepo milele.


Sikia wimbo huu, Mapenzi

Mapenzi ni zaidi ya fikra,
Mapenzi ni kama mchezo,
Mapenzi ni zaidi ya chochote juu yako,

Kwa kila kitu na siku zote,
Mapenzi kama zaidi ya tabasamu tamu,
Mapenzi ni kama wimbo mtamu,

Mapenzi ni zaidi ya hisia,
Ni zaidi ya mawazo,
Mpenzi nibebe tuwe pamoja kama kumbikumbi,

Nakupenda kwa MOYO ,
Mwiliwangu na damu yangu nitakupa,
Napenda unavyonionesha njia za mapenzi,

Hakika sijiwezi kwa mapenzi yako,
Nakumbuka wakati tukiwa pamoja,
Nakumbuka jinsi unavyonitazama,

Nakumbuka unavyoniambia, nikushike,
nikulambe nami nilifanya, kiba hiyana,
Hakika nakupenda kwa kila hali,

Endelea kuniita MPENZI nani nikuite ASALI,
Nakutamkia tena na tena, NAKUPENDA,
Na siwezi kukusaliti milele.


Haiba ya Moyo

Ni kweli wewe ni mwanamke wa pekee,
Umebarikiwa mambo mengi matamu pekee,

Ndimi zako laini, tamu zisizo na mfano,
Mguso wako ni waajabu na wenye ubaridi,
Nikiwa nawe napoteza kumbu kumbu,

Nakiri kusema nikiwa nawe ni zaidi ya mbumbumbu,
Mapigo ya moyo wako yanadunda kifuani mwangu,

Sawa na upepo baharini usiokoma kuvuma,
Nakuwaza kila iitwapo asubuhi,

Na hunijia ndotoni nyakati za usiku,
Nguvu ya mapenzi yako ni zaidi ya silaha za sumu,

Na kamwe siwezi kusimulia utamu wa hazina ya asali yako,
ILA NITAKUPENDA daima.


Mwanamke wa maisha nyangu

Wewe ni mwanamke wa maisha yangu,
Wewe ni Malkia ndani ya moyo wangu,

Mimi ni madini kwenye ngao kichwani mwako,
Wewe ni Jua liwakalo na kunipa mwanga mchana,

Pia hunipa joto nyakati za usiku,
Kadhalika u-miale ya jua la subuhi,

Unataka nikwambie nini kipya?,
Naam pokea ujumbe huu kutoka kwangu wakati huu,

Mimi ni mawingu sahihi ndani ya kifua chako kitamu,
Mimi ni mto upishao maji halisi na masafi yaitwayo MAPENZI, Umenielewa?

Wewe ni mlima wenye kilele kirefu ulijaa kila ainaya raslimali, Japo mmiliki ni mimi lakini wengu wanalitamani,

Naahidi kukulinda na kila aina ya uvamizi dhidi yako,
Sitaki mtu afyeke na kuchoma moto msitu wako wa uletao mmvua iitwayo mapenzi,

Jina lako

Nimeandika jina lako angani,
Lakini mawingu yanelibeba,

Nimeandika jina lako hewani,
Lakini upepo umelichukua,

Nimeandika jina lako katika MOYO wangu,
ambalo lipo na litaendelea kuwepo milele.




Sunday, January 6, 2008

Tenga aichongea Simba Ethipia

Na Fatma Amri

Rais wa Baraza la vyama vya soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, (CECAFA) Leodger Tenga, anaonekana kuichongea timu ya Simba kwa wapinzani wao Timu ya Awasa ya Ethiopia baada ya aliyekuwa mpinzani wa kwenye uchaguzi wa baraza hilo Ashibel Georgis kuwasaidia wapinzani wa Wekundu hao wa Msimbazi.

Aliyekuwa mpinzani wa Leodger Tenga katika kinyang’anyiro cha kuwania urais wa Shirikisho la vyama vya soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Ashibel Georgis amelipiza kisasi kwa kuiweka kambini Timu ya Awasa ya Ethiopia kwa ajili ya kuhakikisha inaifunga Simba.

Akizungumza na Championi, mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, afisa mmoja wa ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia ambaye hakupenda kutajwa jina lake, alisema kuwa Ashibel ameiweka Awasa kambini na kupa kila aina ya msaada ili kuishinda Simba ikiwa ni sehemu ya kulipiza kisasi kwa Tenga baada ya kumshinda katika uchaguzi wa baraza hilo.

Vile vile afisa huyo alifafanua kuwa Simba wanakazi ya kufanya ili kushindwa ugenini kwani tajiri huyo anaendelea kusuka mipango ili kuhakikisha kwamba wawakilishi hao wa Tanzania wapati chochote watakapokuwa ugenini.

Moja ya mipango hiyo ni kuangalia kama kuna uwezekano mchezo huo ukafanyika katika Uwanja wa Awasa ambao historia inaonesha kwamba hakuna timu kutoka nje iliyoshinda katika dimba.

Ili kuonesha hasira zake za kukosa urais wa Cecafa, Ashibel amejitolea kutoa kila aina ya msaada ambao unatakiwa ili kuipa nguvu timu hiyo jambo ambalo litaiwezesha kujiweka vyema kabla ya kukutana na Simba.

Uwanja wa Awasa ni moja ya viwanja vibovu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati kutokana na kuwa na mabonde mabonde hivyo kufanya timu ngeni kuwa na kazi ya ziada kuzoea mazingira katika muda mfupi.

Lakini kwa upande wa mlinzi wa Simba na Taifa Stars, Victor Costa aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu kuwa anaufahamu kwa undani uwanja huo hivyo Simba wasitarajie mteremko katika mchezo dhidi ya Awasa.

Timu ya Awasa ya nchini Ethiopia imepangwa kucheza na Simba katika michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika mchezo utakaofanyika Februari mwaka huu, huku Yanga nayo ikiwa na kibarua kigumu cha kuwakilisha nchi katika michuanoa ya Kombe la Shirikisho.

TAHA kama TAFCA

Na Chausiku Omary.

Kumbe chama cha mpira wa mikono nchini (TAHA) mwenendo wake ni kama chama cha makocha wa soka nchini TAFCA kutokana na kuendesha elimu kwa makocha wao.

Akizungumza na Championi mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama hicho David Mataka, alisema kuwa mafunzo hayo yataendeshwa kwa muda wa wiki moja kwenye Kanda tano tofauti kwa kuwashirikisha waalimu na waamuzi wa mchezo huo.

"Kozi hizo zinalenga walimu na wa mchezo huu kutoka shule za msingi na vyuo tunahitaji ushirikiano wao zaidi ili kuweza kufanikisha mafunzo hayo" alisema Mataka.

Mataka alizitaja kanda zitakazoshiriki katika mafunzo hayo kuwa ni Kanda ya Mashariki, Kusini, Kati, Ziwa na Kaskazini.

Mwanza, mikino hiyooo yaja!

Na Shufaa Lyimo

Wakazi wa mkoa wa Mwanza mpo? haya mashindano ya mikono kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, yanatarajia kufanyika Agast 25 mwaka huu yaha Rock City.

Akizungumza na Championi mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Samaal, Katibu wa chama cha mpira wa mikono nchini (TAHA) Saidi Omary, alisema kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa muda wa wiki moja kwa lengo la kufuzu klabu bingwa ya Africa.

"Mwezi Agast kutafanyika mashindano ya kufuzu klabu bingwa Afrika, ambapo yatashirihisha klabu kutoka nchi 14" alisema Omary.

Said alizitaja nchini ambazo zilizothibitiosha kushiriki katika mashindano hayo kuwa ni Sudan, Comoro, Djibut, Somalia, Zanzibar, Tanzania Bara ,Uganda, Rwandwa, Kenya, Burundi na Zambia wakati Malawi, Zimbabwe, Mourisious bado hazijathibitisha ushiriki wao.

Duh! Simba kila kona!

Mwenyekiti wa Simba ya Jijini Dar es Salaam, Mwina Kaduguda a.k.a Simba wa Yuda.

Na Khamis Bwanga, Kilindi

Kama ulikuwa hujui jinsi mnyama Simba alivyo hatari na mwenye nguvu basi soma habari hii kwa makini ili kujua nini kitatokea kwa mwaka huu.

Akizungumza na Championi mwishoni mwa wiki iliyopita wilayani Kilindi mkoani Tanga, Makamu Mwenyekiti wa Simba Omar Gumbo, alisema kwamba wameazimia kufungua matawi katika kila tarafa na kata kwa nchi nzima ili kuongeza wanachama.

"Ili kujiimarisha tumeamua kufungua matawi nchi nzima lengo ni kuongeza wanachama, na kwamba katika safari yangu hii ya Wilaya ya Handeni nimefungua tawi jipya na sasa tunatarajia kunzunguka nchi nzima kwa ajili ya zoezi kama hilo," alisema Gumbo.

Mwenyekiti huyo wa Simba yupo katika ziara ya mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara kwa ajili ya kuhamasisha zoezi la uandikishaji wa wanachama wapya zoezi ambalo litaendelea nchi nzima.

Yanga-Tumerudi na silaha za maangamizi

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Imani Maugila Omar Madega akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari nchini hivi karibuni.

Na Adolph Balingilaki, Julius Kihampa

Baada ya kurejea nchini kutoka katika ziara ya kimafunzo kikosi cha wachezaJI 27 wa Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam kimeahidi kufanya maangamizi makubwa katika mzungumko wa pili wa Ligi kuu Tanzania Bara na michuano ya kombe la Shirikisho ya Afrika.

Akizungumza na Championi juzi katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam,Nahodha wa timu hiyo,Fred Mbuna alisema kuwa kile walichoenda kukifanya kimekamilika wanachosubiri ni kuingia vitani na kuanza kushambulia maadui wanaowazungumka.

"Kazi tukiyotumwa tumeikamilisha tunasuburi kuanza kushambulia kila adui atakayekuja mbele yetu,huu sio wakati wa kuzungumza maneno matupu tunaingia vitani tukiwa na lengo moja kushinda vita"alisema Mbuna.

Nahodha huyo aliyeongoza kikosi cha vijana wa Jangwani kikiwa chini ya Kocha Mkuu Dusan Kodic akiwa na msaidizi wake Spaso Sokolovski aliongeza kuwa wakiwa nchini Afrika Kusini wamepata mbinu mpya za kupigana sehemu yoyote ya uso wa dunia.

Mbuna alisisitiza kuwa wachezaji wamekuwa makini na mafunzo waliyokuwa wakipewa na walimu huku wakiwa na kumbukumbu ya kutaka kumaliza uteja wa kufungwa na watani wao wa jadi Simba.

"Dawa ya Simba tumekuja nayo kutoka Bondeni,siwezi kusema jina lake lakini nakuomba usubiri mambo makubwa mwaka huu,atuwezi kuwa wataja wa watu wanaolia njaa kila siku, hiyo iatkuwa dharau na mungu apendi"alisisistiza Mbuna.

Naye Katibu Mwenezi wa Yanga,Francis Lucas akizungumza na Championi alisema kuwa nia na malengo ya safari yametimia wanachosubiri ni vijana kuanza kufuna walichopanda katika ardhi yeye rutuba.

"Tumetumia gharama kubwa kuweka kambi kuanzia Mwanza hadi huko nchini Afrika Kusini,tunataka kuona kile ambacho tumekipanda kama kitaota kama tunavyotaka,wakati wa ubabaishaji umekwisha tunataka mafanikio zaidi"alisema Francis.

Katibu Mwenezi huyo aliongeza kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Dusan Kodic hakupenda kucheza mechi ngumu kutoka na kutaka wachezaji wake waweze kupata maelekezo yake kwa ufasahaz zaidi.

Timu ya Yanga imerejea nchini ikiwa na kibarua kigumu cha michuano ya kombe la Mapinduzi inayoanza kesho katika dimba la Amani huko Tanzania Visiwani(Zanzibar) huku ikisubiri kuanza mchakamchaka ya duru la pili la Ligi Kuu Tanzania Bara Januari 26 mwaka huu.