Sunday, May 11, 2008

Kwa hili la Nyamagana JK anasalitiwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) wakati Rais Kikwete alipotembelea nchi hiyo hivi karibuni. Picha kutoka kwenye mtandao wa www.gov.rw.




Picha ya kwanza (juua) inaonesha kitambulisho cha jiji la Mwanza jiji ambapo unatatikana uwanja wa Nyamagana, chini ni Ramani ya Tanzania ikionsha jiji la hilo. (Picha kutoka mitandao mbali mbali).


Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Kwanza napenda kushukuru Mungu kwa kunipa uhai hadi hivi sasa kwani sikustahili bali ni kwa rehema zake pekee.

Vile vile naomba anipe hekima za kuweza kufafanua jambo ninaloliona linasumbua jamii yetu hasa kwa wakazi wa jiji la Mwanza nalo ni uwanja wa michezo wa Nyamagana.

Uwanja wa michezo wa Nyamagana uliopo jijini Mwanza upo katika mchakato wa kufanyiwa mabadiliko katika matumizi yake kwa kile kilichoelezwa kuwa kufanywa kitega uchumi ikiwemo maegesho ya magari na kujengwa hoteli.

Hatua hii Halmashauri ya jiji la Mwanza kufanya mabadiliko katika matumizi ya uwanja huu yameonekana kupingwa na wadau mbali mbali wa michezo nchini kwa kile walichoeleza kuwa ni kurudisha nyuma jitihada za kuinua michezo.


Kimsingi jiji kama mamlaka inayosimamia shughuli za kila siku za kimaendelea ndani ya Mwanza walikuwa na sababu ya kufanya mabadiliko katika maeneo mbali mbali lengo likiwa kuboresha hali ya mazingira na kupamba jiji hilo ili kuvutia kama yalivyo majiji mengine duniani.

Kadhalika uboreshaji ambao jiji wanataka kuufanya yawezekana ukawa na manufaa katika uchumi wa jiji lakini ninaimali suala hili limefanyika pasipo upembuzi yakinifu hivyo katika hali hii ambayo imefikia.


Umakini ama upembuzi yakinifu ninaoungumza ni wakimaamuzi ambao watendaji wa halmashauri ya jiji la hawakuufanya ambapo pamoja na mambo mengine lakini wadau wa michezo mbali mbali walistahili kushirikishwa kabkla ya kufikia uamuzi kutokana na uwekweli kwamba wameutumia uwanja huo kwa miaka mingi.

Ikumbukwe kwamba Uwanja wa Nyamagana umekuwa ukitumiwa na taasisi mbali mbali zilizopo jijini Mwanza kama shule za msingi na sekondari, vyuo, mashirika ya serikali na yasiyokuwa ya kiserikali katika shughuli za michezo kwa miaka mingi.

Wengi tunafahamu historia ya uwanja huu ambao ni moja ya viwanja vya zamani zaidi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo wazawa na wasiokuwa wazawa wa mkoa wa Mwanza wameutumia kwa miaka nenda rudi.


Kutokana na hali hiyo nachelea kusema kwamba watendaji hawa wameshindwa kutekeleza kwa vitendo kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete juu ya matumizi ya viwanja vya michezo.

Kumbu kumbu zangu zinanionesha kwamba umakini na Rais Kikwete katika kusimamia matumizi ya viwanja vya wazi na vya michezo yalichangia kwa kiasi kikubwa kureshwa kwa baadhi ya viwanja vilivyokuwa vinavyemelewa na matajiri kwa ajili ya shughuli za gereji, maegesho ya magari na matumizi mengine.

Kwa mfano Uwanja wa Kigongo chekundu Manzi mmoja jinini Dar es Salaam, ni miongoni mwa viwanja vilivyokuwa katika katari ya kupotea kutokana na kuanza kuvamiwa lakini baada ya kauli ya JK katika masuala ya viwanja hakuna aliyeegesha gari katika uwanja huo tena.

"....viwanja vya wazi vibaki kwa ajili ya matumizi husika, na yule mtu tajiri anayehiona anauwezo akanunue nyumba aiboe kati kati ya mji ili apate sehemu ya kuegesha magari yake..." hii ilikuwa ni sehemu ya kauli ya rais katika moja ya hotuma zake akioneshwa kukerwa na hali hiyo.

Matumizi ya Uwanja wa Nyamagana yameonekana kupingwa na wenyeji na wakazi wa Mkoa Mwanza kwa kila aina ya nguvu ambapo imefikia hatua ya watu kuandamana kuonesha hisia zao.

Maandamo yale hayakuwa ya bure bali yalikuwa na umuhimu na ujumbe mzito hasa kutokana na kuwashirikisha watu wa rika mbali mbali, kwa mfano Wazee, Vijana, Watoto na Wanafunzi wanaosoma katika shule na vyuo mbali mbali ndani ya Rocky City kama wengi wanavyoliita.

Naamini kuwa ni mtu Mwendawazimu au Mchawi ndiye anaweza kupinga maendeleo yanayolenga kuinufaisha jamii na Taifa, hii inaama kwamba kama matumizi ya Uwanja wa Nyamagana kama yangelenga kuleta tija katika maendeo ya Wanamza na Tanzania kwa ujumla.

Lakini maandamano ya hivi karibuni yamelenga kuonesha hali halisi kuwa nini wakazi wa Mwanza wanahitaji katika sakata hili.

Maamini na nitaendelea kuamini kiwamba kwa manma moja ama nyingine wakazi wa jiji la Mwanza ni watu wenye akili timamu na hawajakurupuka kuchukua uamuzi walioufikia ikiwemo kufanya maandamano.

Pia ninaamini kwamba Rais Kikwete hakutendewa haki na kauli zake zimekiukwa wazi wazi na kama si kusalitiwa na watu wachache.

Ung'ang'anizi unaofanywa halmashauri juu ya suala hili unazusha masuali mengi yasiyojibika kwamba nini maslahi kwa Taifa juu ya suala hili, kwa kuwa kama ningeulizwa maslahi ya Taifa kama uwanja huo utabakia kama ulivyo sasa ni kwamba vipaji vya watoto wetu na wanamichezo wa zamani haviwezi kutoea na vitafaa katika siku zijazo.

Lakini suala hili hata Wazara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ililiona kuwa kulikuwa hakuna haja ya kuufanyia mabadiliko uwanja huo na ndiyo maana iliharamisha matumizi yake.

Hili ni jambo la kusikitisha kuona kwamba licha ya juhudi zilizooneshwa na wakazi wa jiji kupinga hatua ya halmashauri kubadilisha matumizi ya uwanja huo, lakini bado wahusika wanaendelea kushikia uamuzui huu ambao wengi hawautaki kwa maslahi ya wengi.

Kama tunafauata misingi ya utawala bora basi huu ndiyo msingi mathubuti na kuonesha kuwa sisi ni watu tuliostarabika kwa kusikiliza nguvu ya umma kuwa inasema nini kwani hii ndiyo temokrasia yenyewe.

Naziomba mamlaka husika kusikia kilio cha watu hawa na msisuburi hadi serikali kuu kuingilia kati au rais atoe kauli kwani ikifikia huko ni sawa na kushindwa kujua wajibu wenu.

Manaamini kuwa huu ndiyo ukweli wa mambo. mamshukuru Mungu kunipa hekima za kunifikisha hapa. Kamwe siwezi kuwa adui wa mtu kwa kusema ukweli.

No comments: