Kondic aiweka Yanga roho juu Na Mwandisho Wetu KOCHA Mkuu wa Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam Dusan Kondic, anatatajia kukaa pamoja na viongozi, Mfadhili Mkuu, Yusuf Manji kwa aliji ya kupanga bajeti ya msimu wa Ligi Kuu ambayo ndani yake kutakuwa na suala zima na usajili.
Akizungumza na Championi jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita, Kondic alisema kwamba hatua hiyo ni maandalizi kwa ajili ya kufanya usajili kabambe kwani katika hatua hiyo kutahitajika vitu vingi muhimu.
Kondic aliongeza kuwa bajeti ya msimu ujao ndiyo itaamua kuchukua wachezaji wa aina gani licha ya ukweli kwamba majina ya wachezaji anatakaowaacha ameshayafahamu.
Alisema kuwa baada ya kufanya mazungumzo ya kila kwa wachezaji ataowaona wanamfaa wataingia mkataba na klabu kwa ajili ya kuwemo kwenye kikosi chake.
Alisema wameamua kuchukua hatua hiyo ili kuhakikisha kwamba wachezaji watakaosajiliwa wanakidhi vigezo wanavyovihitaji hivyo uwezo wa mchezaji husika kuwa lipo juu kiasi gani.
"Hadi hivi sasa sijaamua nimchukue nani kutokana na ugumu wa wachezaji ulipo kwa sababu bado naangalia lakini naweza kuthubutu kusema kwamba ni mapema mno kusema chochote.
"Kwa sasa tupo katika hatua nzuri ya kuandaa mikataba hivyo natarajia kukutana na viongozi, mfadhili ili kuweza kupanga bajeti ambayo itaamua kila kitu kuhusiana na suala zima la usajili", alisema Kondic.
Kocha huyo alisema kuwa mabadiliko katika kikosi chake yatategemea kupatikana na kwachezaji wapya kutoka sehemu mbali mbali nje na ndani ya nchi.
Kuhusiana na achezaji kutoka nje ya Tanzania kijiunga kwenye kikosi chake, Kondic alisema kwamba bado hawezi kuzungumza lolote kwani bado huyo katika mchakato wa wachezaji wa ndani, hivyo baada ya michuano ya Kombe la Taifa ndio atajua kila kitu.
"Kwa sasa naangalia zaidi wachezaji wa ndani, kuhusiana na wachezaji wa nje ya Tanzania bado ninaendelea kufanya mawasiliano nao ila siwezi kuwataja majina moja kwa moja naomba uvute subra utajua kila kitu", alisema Kocha huyo.
Mipango ya kupanga bajeti, kuandaa mikataba huenda ikawa ni donge nono la kuendelea kuwabakisha wachezaji wachanga kama Jerry Tegete, na Mrisho Ngassa kuendelea kuwika ndani ya mitaa ya Jangwani na Twiga.
Katika hatua nyingine Kondic amesema kwamba amekubali kumuachia, Athmani Idd 'Chuji' ili aende kucheza soka la kuliopwa barani Ulaya.
"Ninafurahi iwapo Chuji anaenda Ulaya lakini nitahakikisha nampa mbinu mbadala za kucheza soka la Ulaya kwani naamini hii itakuwa ni sehemu muhimu katika maisha yake, vile vile nawataka wachezaji wengine wajiandae kucheza soka la kimataifa kwa kuwa maanini wanaweza kufanya hivyo" alisema Kondic.
Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za mchezaji huyo kwenda Ulaya kufanya majaribio ya soka la kulipwa, lakini hapo kakla Klabu ya Al Akhdar ya Libya ilionesha kuwanyatia nyota huyo sambamba na Jerry Tegete, Ngassa, Abdi Kassin ambao wote wanakipiga katika Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
No comments:
Post a Comment