Sunday, May 11, 2008

TFF yazikaanga Simba, Yanga

Mwakabela

Mwandishi Wetu

Shirikisho la soka nchini TFF linatarajia kuanzisha kanuni mpya kwa ajili ya usajili wa wachezaji wakigeni kanuni ambazo huenda zikazibana au kuzisaidia timu za Simba na Yanga katika mbio zake za usajili msimu ujao.

Akizngumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela alisema kwamba wameamua kuchuanzisha kanuni mpya za usajili wa wachezaji wa kigeni ili kuwa na wachezaji wenye viwango vinavyotakiwa.

Alitaja taratibu mpya ambazo wachezaji wa kigeni watatakiwa kuwa nazo kuwa ni cheti au leseni ya Ligi Kuu katika nchi husika au awe nacheza katika Timu ya Taifa bila kujali aina niya umri gani.

"Wachezaji wa kigeni ambao wataweza kusajili ni wale wote wenye cheti cha Ligi Kuu katika nchi husika au awe katika kikosi cha Timu ya Taifa kwa kudhibitishwa na uongozi wa shirikisho la nchi yake, vinginevyo usajili wake utakwama", alisema Mwakalebela.

Alisema kwamba wameamua kuanzisha kanuni hizo ili kuepusha wachezaji wasiokuwa na sifa kukimbilia katika klabu za Tanzania wakiwa na imani kuwa wanaweza kupata nafasi ya kucheza soka kwa kigezo kuwa yeye ni mgeni.

Kanuni hizo zinaweza kuzikaanga au kuzisaidia klabu za Simba na Yanga ambazo mara kadhaa zimekuwa zikisajili wachezaji wa nje ambapo wengine wamekuwa hawana viwango vinavyostahili kuitwa wachezaji wa kulipwa.

No comments: