Saturday, April 19, 2008

JIMAMA FUSKA LANASWA

Kutoka, http://www.globalpublisherstz.com
Jimama moja ambalo ni mke wa mtu, limenaswa likijiuza kupitia picha yake chafu aliyopiga akiwa nusu uchi na kuisambaza kwenye mtandao kwa nia ya kutafuta wateja.


Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, jimama hilo ambalo limeamua kumsaliti mumewe limebainika kuwa liko katika ndoa changa ya mwezi mmoja na mumewe yuko masomoni Uingereza.


Chanzo chetu cha habari kimenasa pia taarifa zake ambazo zinamtaja kuwa, ni mfanyakazi wa kampuni moja kubwa ya simu za mkononi jijini Dar es Salaam (jina tunalihifadhi).


Mwanamke huyo anadaiwa kufanyakazi katika kitengo cha huduma kwa wateja (customer care) huku makazi yake yakiwa eneo la Ocean Road na kufahamika kwa jina linaloanzia na herufi G.


Picha hiyo iliyotumwa katika mtandao wa kompyuta ‘internet’ na jimama hilo kwa staili ya kuonyesha ‘karibu mteja’ inamuonyesha akiwa amelala kifudifudi chumbani nusu uchi (makalio yake yakiwa matupu), huku akibofya kompyuta ndogo (laptop).


Katika picha ya jimama hilo kulikuwa na maelezo yaliyokuwa pamoja na namba yake yake ya simu ya mkononi.


“Nimeona picha ya ...(anamtaja jina), iko kwenye mtandao, ni yeye kabisa kwani namfahamu, lakini anakosa nini kwa mumewe? Kuna sababu si bure,” kilitonya chanzo chetu cha habari huku kikionekana kustaajabishwa na vituko vya jimama hilo.


Habari zaidi zinasema kuwa, mwanamke huyo alikuwa katika maandalizi ya kumfuata mume wake masomoni Uingereza, ili kwenda kuimarisha ndoa yao changa.


“Inavyoonekana ‘mdada’ mwenyewe kicheche, hajatulia na hawezi kuvumilia hata kwa wiki,” kilisema chanzo chetu.


Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja sababu hasa ya mwanamke huyo kuamua kutafuta wanaume wa muda (part time) wa kujirusha nao wakati anapata mahitaji yote muhimu kutoka kwa mumewe.


Haijajulikana pia kama mwanamke huyo hajui kuwa kuanika picha yake mtandaoni kunaweza kumfanya mumewe aione akiwa huko huko Ulaya.


“.....au jamaa nae kampiga chini? Sintashangaa sana kwani mtoto hajatulia kabisa kuwa mke, juzi juzi jamaa yangu (anamtaja kwa jina) alikuwa anachukua kwa saana! Pole zake mumewe.............!. Kilimalizia chanzo chetu hicho.


Kwa kutumia namba ya simu iliyowekwa katika picha yake, mwandishi wetu alimpigia na kupokelewa na mwanamke ambaye alipoulizwa kama yeye ni G, alikanusha.


Aidha, alikanusa kufanyakazi katika kampuni ya simu iliyotajwa katika maelezo yaliyoandikwa katika picha hiyo.


Licha ya kukanusha, baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo waliongea na mwandishi wetu baada ya kuinasa picha hiyo mtandaoni, walithibisha kuwa ni yeye.

No comments: