Sunday, July 1, 2012

DK. ULIMBOKA ASAFIRISHWA NJE YA NCHI KWA MATIBABU


Baadhi ya watu wakiangalia gari lililombeba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini Dk. Steven Ulimboka katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam wakati alipokuwa akienda kupata matibabu nje ya nchi baada ya madaktari wenzake kuchangishana fedha.  Wanaharakati mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa habari wanawake (TAMWA) Ananilea Nkya wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali wakati walipomsindikiza Mwenyekiti wa jumuiya ya Madaktari nchini Dk.Steven Ulimboka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati alipokuwa akienda kupata matibabu nje ya nchi.

No comments: