Kampala, Uganda
WATU kadhaa wanahofiwa kufariki dunia katika maporomoko ya arthi Mashariki mwa Uganda. Hii ni kwa mujibu wa maafisa eneo hilo.
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini
Uganda limeambia BBC nyumba 15 zimefunikwa na udongo katika wilaya ya Bududa.
Vijiji vilivyoathirika ni karibu na
Mbuga ya Mlima Elgon ambayo hutembelewa na watalii karibu na mpaka na Kenya.
Shirika la Msalaba Mwekundu limetuma
kikosi cha wokozi eneo hilo kutathmini uharibifu.
Katibu wa Shirika la Msalaba
Mwekundu Uganda Michael Richard Nataka ameambia BBC kwamba katika kijiji komoja
nyumba 15 zimefunikwa huku watu wengi wakikwama kwenye makaazi yao huko Bududa.
Tayari watu 20 wamethibitishwa kufa
na idadi hii huenda ikaongezeka.
Awali maafisa walisema watu kati ya 20 hadi 100 waliangamia. Eneo hilo limeshuhudia mvua kubwa katika siku za karibuni.
Awali maafisa walisema watu kati ya 20 hadi 100 waliangamia. Eneo hilo limeshuhudia mvua kubwa katika siku za karibuni.
Hapo Agosti mwaka jana watu 24
walikufa baada ya mvua kubwa kusababisha maporomoko ya arthi katika Wilaya ya
Bulambuli Mashariki mwa Uganda. Mwaka 2010 watu 100 walikufa katika Wilaya
Bududa baada ya maporomoko ya arthi.
No comments:
Post a Comment