Friday, January 23, 2009


Joseph Kabila
Paul Kagame

Nkunda

Kiongozi wa waasi katika Jamhuri ya Kongo Generali Laurent Nkunda (pichani chini) ambaye kwa muda mrefu amekuwa akiisumbua Serikali ya (DRC) inayoongozwa na Joseph Kabila, hatimaye amekamatwa Alhamisi usiku na majeshi ya Serikali ya Rwanda wakati akitaka kuvuka mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Taarifa za awali zilisema kwamba Nkunda alikuwa akitaka kutoka katika ngome yake iliyopo mashariki mwa Kongo baada ya kutokea mashambulizi makubwa yaliyofanywa na majeshi ya Serikali ya Kongo pamoja na yale ya Rwanda hivyo kuona njia pekee ilikuwa ni kukimbilia Rwanda.

Wachunguzi mambo wanasema kwamba Nkunda inawezekana kwamba ameuzwa baada ya kutokuwepo maelewano baina ya maswahiba zake ambao awali walikuwa wakijulikana kuwa ni serikali ya Rwanda.

Tayari serikali ya DRC imeomba kupelekwa Nkunda ndani ya Kongo ili akastakiwe kutokana na makosa ya kivita alioyoyafanya wakati wa mapigano huku tuhuma kubwa zikiwa ni zile ubakaji wa wanawake na watoto, mauaji pamoja na utumikishaji wa watoto katika vita.

Kwa habari zaidi na kujua nini hatua itachuliwa baada ya kukamatwa kwake endelea kubofya katika mtandao huu wa wazalendo.